Ezekiel 27:1-6

Maombolezo Kwa Ajili Ya Tiro

1Neno la Bwana likanijia kusema: 2 a“Mwanadamu, fanya maombolezo kwa ajili ya Tiro. 3 bUmwambie Tiro, ulioko kwenye lango la bahari, ufanyao biashara na mataifa mengi ya pwani, ‘Hili ndilo Bwana Mwenyezi asemalo: “ ‘Ee Tiro, wewe umesema,
“Mimi ni mkamilifu katika uzuri.”

4 cMipaka yako ilikuwa katika moyo wa bahari,
wajenzi wako walikamilisha uzuri wako.

5 dWalizifanya mbao zako zote
kwa misunobari itokayo Seniri;
Yaani Hermoni.

walichukua mierezi kutoka Lebanoni
kukutengenezea mlingoti.

6 fWalichukua mialoni toka Bashani
wakakutengenezea makasia yako;
kwa miti ya msanduku
kutoka pwani ya Kitimu
wakatengeneza sitaha
Yaani sakafu ya merikebu au mashua.
yako
na kuipamba kwa pembe za ndovu.
Copyright information for SwhKC